Wikiendi Live 2025 - Fomu ya kutuma maombi ya msanii/Kikundi
Bado tu hamja apply WIKIENDI LIVE imeitika! link ya kujiunga hii apa!
Kiswahili
https://docs.google.com/forms/d/e/1FAIpQLSeD7oUD5itg1hMv7eqPBlOWvpw4p1_3VLVHTY6RKlo4QoyCiA/viewform
English
KUHUSU NAFASI ART SPACE
Nafasi Art Space ni kituo cha sanaa na Utamaduni asili na kisasa kilichopo Dar es Salaam, Tanzania. Tunatoa fursa kwa wasanii wa fani aina zote kuunda, kujifunza, kubadilishana mawazo, kuonyesha kazi zao, na kuonesha vipaji vyao. Kupitia programu zetu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na, warsha, mazungumzo ya sanaa, maonyesho ya filamu, maonyesho ya sanaa, matamasha, na maonyesho ya sanaa ya umma, tunalenga kuongeza na kukuza uwezo wa kibinadamu kupitia sanaa ya kisasa.
Jina Nafasi leye maana nyingine ya “Fursa” , Nafasi inajitahidi kuwa kituo kinachotoa fursa kwa wasanii wachanga na wabobezi kujifunza na kutengeneza kazi za sanaa zenye kuunganisha ,kusisimua, na kuburudisha hadhira kupitia majukwaa huru,warsha za kuongeza ujuzi na ufundi katika tasnia ya sanaa na Utamaduni.Nafasi Art Space inajithidi kuongeza chachu ya ubunifu na kuuwa jukwaa mahususi kwa wasanii wa changa na wabobezi kuonyesha utajiri na kuendeleza uwezo wa binadamu kupitia sanaa za kisasa, Nafasi Art Space inajitahidi kuwa kitovu cha ufanisi kinachopromoti ubunifu na weledi wa wasanii wa kisasa wa Kitanzania kupitia mafunzo, kuwapa nafasi ya kujitangaza, mazungumzo ya kitamaduni ya kimataifa, na ushirikiano katika kazi za sanaa.
Tunayo furaha kuwatangazia wito rasmi wa kushiriki kwa wasanii wachanga na waliobobea wa kazi za sanaa za jukwaani, pamoja na watu wengine wenye vipaji na shauku ya kuonesha kazi zao za muziki pamoja na dansi kwa hadhira kubwa, katika tukio la "WIKIENDI LIVE" 2025,Hii ni moja ya fursa pekee kwa wasanii kupata fursa kuonyesha kazi zao kwa hadhira, kuungana na wasanii wenzao kwa manufafaa ya kuendeleza saana zao.
KUHUSU WIKIENDI LIVE
WIKIENDI LIVE ni tukio la kipekee na mahiri la muziki mubashara linalotolewa kwa ajili ya kuonesha midundo ya kiafrika na iliyochanganywa na aina tofauti tofauti za muziki. Jukwaa hilinajumuisha wasanii kutoka kote Tanzania na Zanzibar, pamoja na wasanii wanaotembelea kikanda na kimataifa ambao huleta fursa zinazopelekea uhamasishaji na kubadilishana mawazona wasanii wa ndani ambao wanafaidika kwa kucheza pamoja na kuingiliana na wanamuziki wa kimataifa walioimarika zaidi. Tukio hilo litaboresha taaluma na kuwajengea uwezo wanamuziki wa Tanzania na wa nje.
Tukio hili linatoa fursa kwa wasanii ambao wapo tayari kujitoa katika mifumo iliyozoeleka na inayotarajiwa kisasa, kwa kuchukua vionjo vya urithi wa ndani, au kujaribu kuja na aina za kiupekee, au vote viwili.
WIKIENDI LIVE ni jukwaa lenye malengo ya kuivutia hadhira yenye kupenda ladha tofauti tofauti na wenye kutaka kuongeza na ujuzi na kuelewa kwa undani kutokana na kushrikishwa katika majukwaa ya muziki ambao unasisimua, unashawishi na kufufua hamu ya utajiri wa muziki wa Afrika Mashariki
Jukwaa la WIKIENDI LIVE linalenga kukuza watazamaji ambao ni wajasiri katika ladha zao na wanaopenda kupanua upeo wao wa muziki kwa kuonyeshwa muziki wa moja kwa moja unaosisimua, kuhamasisha, na kufufua shauku kwa urithi wa muziki wa Afrika Mashariki.
Tukio la WIKIENDI LIVE huandaliwa na Nafasi Art Space jijini Dar es Salaam kila mwaka (Septemba) pamoja na maonesho shirikishaji ya sanaa yajulikanayo kama CHAPCHAP (www.nafasiartspace.org), kwa msaada kutoka kwa Ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Uswizi na Baraza la Sanaa la Taifa la Tanzania.
Wasanii wote wanaopenda kushiriki katika tukio la WIKIENDI LIVE tarehe 26 na 27.09.2025 wanahitajika kukamilisha fomu ya maombi mtandaoni. Waombaji lazima watembelee Nafasi Art Space kwenye mitandao ya kijamii ili kupata fomu ya maombi pia kusoma na kuelewa kwa umakini Mpango Mkakati wa Nafasi Art Space 2021/26. Muda wa mwisho wa kukamilisha maombi ni saa sita usiku (EAT) tarehe 28/03/2025.
Vigezo vya kushiriki:
1. Taaluma za kisanii zinazohusiana na tasnia ya muziki/muziki mubashara.
2. Tunathamini vipaji na tunahimiza wasanii kuonyesha ubunifu wa kuvutia na wenye kuvuta fikra. Uzoefu wa sanaa unathaminiwa, lakini pia tunakaribisha wasanii wenye viwango tofauti vya uzoefu wanaoonyesha shauku na kujitolea kwa fani yao.
3. Tunahimiza sana wasanii kutoka asili tofauti kuomba, ikiwa ni pamoja na makundi yaliyotengwa na jamii zisizowakilishwa ipasavyo, ili kushiriki sauti zao.
4. Waombaji wanapaswa kuwa tayari kushiriki kikamilifu katika tukio hili la burudani zitakazokua mubashara kabisa.
5. Waombaji wanapaswa kuwa raia wa Tanzania wanaoishi Dar es Salaam. Wasanii au makundi yanayokaa nje ya Dar es Salaam, Afrika au wasanii wa kimataifa wanaweza kuzingatiwa, lakini wana wajibu wa kujigharamia kifedha kwa usafiri na malazi yao. Nafasi Art Space itasaidia katika mchakato wa visa kwa kutoa barua za mwaliko rasmi.
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi;
performingarts@nafasiartspace.org cc info@nafasiartspace.org
+255 757 820 426 // +255 757 406 258
Tembelea Nafasi Art Space, Eyasi Road Industrial Area , Mikocheni B